duniani, "The greatest food on Earth", na
FDA (U.S. Food and Drug Administration) iliielezea spirulina kuwa ni chanzo bora cha protini cha binadamu.
Shirika la Chakula Ulimwenguni (FAO) ilisema kuwa spirulina ni chakula bora zaidi cha karne ya 21.
Spirulina ndicho chakula cha wanaanga wa NASA.
Spirulina ni kiumbe wa kale wa majini mwenye umri unaolingana na bahari yenyewe. Ni kitu chenye rangi ya kijani-bluu kinachofanana na mwina, kinachoelea juu ya maji, ambacho pia hujulikana kwa jina na cyanobacteria kwa sababu ya rangi yake na vinasaba vyake vinavyofanana na vile vya bakteria. Spirulina huishi kwenye maji ya chumvi na kwenye maeneo ya dunia yenye maziwa ya maji ya joto yenye alkali za volkano. Spirulina ina chlorophyll na hutumia jua kama chanzo chake cha nishati, kama ifanyavyo mimea na alga. Wanasayansi wanaipenda sana kwa sababu ya uwingi wa lishe iliyo ndani yake yenye sifa za kipekee.
Manufaa Ya Spirulina Kwa Lishe
1. Mafuta Kidogo:
Spirulina ina kiwango kidogo sana cha mafuta (low saturated fat) na kuifanya kuwa chanzo bora cha chakula kwa jamii ya leo inayotatizwa na unene wa kupindukia
2. Kiasi kukubwa cha protini na mafuta yasiyoganda (unsaturated fatty acids)
Kiasi cha protini ndani ya spirulina kinafikia hadi asilimia 60-72 ya uzito wake baada ya kukaushwa na gramu 1 ya spirulina inaweza kutosheleza mahitaji ya protini ya mtu mzima mwenye afya kwa asilimia 60 hadi 70. Mafuta (unsaturated fatty acids) ndani ya spirulina yana faida kwa watu wenye cholesterol kwa wingi (hypercholesterolemania) na wenye mafuta kwenye mishipa ya damu (atherosclerosis), msongo kabla ya hedhi na arthritis na ni kiambata cha kupunguza uzito.
3. Wingi Wa Vitamini, Madini na Antioxidants
Kiujumla, gramu 1 ya spirulina ina lishe sawa na kilo 1 ya mboga na matunda. Ina kiasi kikubwa cha ferrous (mara 20 zaidi ya chakula cha kawaida chenye ferrous kwa wingi kama spinach). ina kiwango cha B12 mara 3.5 ya kile kilichomo ndani ya maini ya wanyama. Ina carotinoids mara 1.5 ya ile iliyomo ndani ya karoti. Kuna mlolongo wa vitamini B zikiwemo B12, vitamini K, na madini kama calcium, magnesium, selenium, manganese, potassium, na zinc.
Spirulina ni chanzo kikubwa cha selenium asilia, ambayo ni anti-oxidant yenye nguvu. Selenium hufanya kazi ikisaidiana na vitamini E kuhakikisha upatikanaji wa oksijeni ya kutosha kwenye misuli na haswa kwenye myocardium. Kinga za mwili pia husaidiwa na selenium. Selenium pamoja na Vitamini E hulinda chembechembe nyekundu za damu, ngozi nyembamba inayozunguka seli na viungo vya seli kutokana na radikali huru. Kitu kikubwa zaidi ni kuwa selenium ni kiungo muhimu cha kimeng'enyo kiitwacho glutathione peroxidase. Kugundulika kwa glutathione peroxidase kulionyesha kwa nini selenium ni kitu muhimu zaidi katika kujikinga na kansa, magonjwa ya moyo, arthritis na kuzeeka kwa haraka. Kazi kubwa ya peroxidase katika mwili ni kuvilinda viungo vya kuzuia madhara ya oksijeni (oxidative damage).
Kuzuia Kansa (Anti-cancer Feature):
Utafiti uliofanywa huko Japan (Hokkaido University Graduate School of Medicine) ulidokeza kuwa uwezo wa spirulina kupigana na uvimbe unaweza kutokana na uwezo wake wa kuzisaidia seli asilia za mwili za kuua vivamizi kutoka nje (Natural Killer cells). Seli asilia za kuua vivamizi zina uwezo wa kutambua vitu kutoka nje vinavyouvamia mwili na kuviangamiza.
Kuwepo kwa kiasi kikubwa kwa chlorophyll na B-carotene katika spirulina kunaweza kueleza uwezo wake wa kuzuia ujengwaji wa makoloni ya kansa kwa sababu vitu hivi hugandana na kusababisha utolewaji wa kemikali zinazosababisha kansa. Ikiwa seli za kansa zitazuiliwa kabla hazijajenga koloni, seli za kansa ambazo kikawaida huwa zimo ndani ya mwili hazitapata nafasi ya kukua na kusababisha ugonjwa wa kansa.
Huko Marekani, The Harvard School of Dental Medicine, kansa ya mdomo iliweza kupunguzwa kwa kutumia spirulina na matokeo kuchapishwa kwenye ripoti ya mwaka 1986.
Uwezo wa kuzuia kansa wa phycobiliprotein iliyopo ndani ya spirulina ulipewa hati miliki USP1150726-A82679 huko marekani na JP58065216 huko Japan.
Kuzuia Madhara Ya Mionzi (Anti-radiation Feature):
Tafiti zimeonyesha kuwa spirulina hutoa kinga dhidi ya mionzi (Radioctivity). Tafiti zimefanywa kutumia watoto wanaoishi kwenye sehemu za dunia zenye mionzi kwa wingi, na matokeo yalionyesha kuwa spirulina inalinda kinga za mwili dhidi ya mionzi na kupunguza viwango vya mionzi kwenye mkojo.
Watoto wa Chernobyl walipewa spirulina na viwango vya mionzi kwenye mikojo yao vilipungua kwa asilimia 50 katika siku 20. Watoto hawa walipewa gramu 5 za spirulina kwa siku kwenye chuo cha utafiti wa mionzi huko Minsk (Belarus Institute of Radiation Medicine).
Hati miliki ya matumizi ya spirulina kama chakula cha kupunguza mzio unaotokana na magonjwa yanayotokana na mionzi ilitolewa huko Urusi mwaka 1994.
Kuzuia Mzio (Anti-allergy Features):
Utafiti wa karibuni uliohusisha watu 36 wenye matatizo ya mafua (allergic rhinitis) ulionyesha kuwa matumizi ya gramu 2 za spirulina kwa siku yalipunguza kiwango cha Interluken-4 (IL-4) katika miili yao. IL-4 hutengenezwa na seli za kinga za mwili na huhusika na utengenenezaji wa antibody, Immunoglobin E (IgE), ambayo huepusha dalili za mzio wa rhinitis.